Psalms 80:8-13


8 aUlileta mzabibu kutoka Misri,
ukawafukuza mataifa, ukaupanda.

9 Uliandaa shamba kwa ajili yake,
mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.

10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,
matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.

11 bMatawi yake yalienea mpaka Baharini,
Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania.

machipukizi yake mpaka kwenye Mto.
Yaani Mto Frati.


12 eMbona umebomoa kuta zake
ili wote wapitao karibu
wazichume zabibu zake?

13 fNguruwe mwitu wanauharibu
na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
Copyright information for SwhKC